Italiano English French Espanol
flash

Edizioni

Questo libro è tradotto in lingua:

Il tuo carrello

Prodotti nel carrello
20
Totale spesa
€ 480,50

Injili kama nilivyofunuliwa - 1

978-88-7987-017-7
Injili kama nilivyofunuliwa - 1

Ni maandiko maalum ya mwandishi huyo anamoeleza maisha yake Bwana Yesu, tangu azaliwe Bikira Maria hadi Kupokea kwake mbinguni. Maandiko haya siyo Injili mpya, lakini ni utimilifu wa yale mapokea manne ya kienjili na ufafanuzi wake. Maria Valtorta aliita kazi hiyo “Habari Njema ya Bwana yetu Yesu Kristu kama Yohane Mdogo alivyofunuliwa”. Kufunuliwa maana mwandishi ashuhudia hakuna asili ya kibinadamu alikoweza kupata aandikalo. Yohane maana mara nyingi huitwa hivi na Bwana Yesu, akimfananisha na yule mwandika Injili, mwanafunzi wake mpendwa. Mdogo maana mwandishi akadiri kazi yake ni ya kufuatana na chini ya ile ya Injili Takatifu.
Kazi nzima imegawika katika taratibu ya pekee ya sura ya kuendelea. Kila sura imegawiwa katika aya nyingi, kila moja yenye maana yake iliyotimilika.
Shabaha ya Kazi hii
Shabaha yametolewa na Bwana Yesu mwenyewe katika imla yake mojawapo kwa mwandishi: “Mapenzi yangu ni kwamba Neno langu lijulikane, lienee, litumike na watakatifu na waamini... Ningependa kwamba kutoka Nchi hii... ulimo Ukao wa Kimitume... Kazi ieneze... kwenye ulimwengu wote wa wakristu-katoliki.
Maandiko mengine
Maria Valtorta aliandika vitabu vingine kadhaa, hasa: “Kitabu cha Azaria” (Kielezo cha kiroho na cha teolojia kuhusu Misa ishirini na nane za sikukuu), na “Maisha yake mwenyewe”.

(Swahili edition - Edition en langue swahili)